Wydad Yafikia Makubaliano na Singida BS Uhamisho wa Seleman Mwalimu

Filed in Michezo Bongo by on January 31, 2025 0 Comments

Wydad Yafikia Makubaliano na Singida BS Uhamisho wa Seleman Mwalimu | Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco imefikia makubaliano na klabu ya Singida Black Stars ya Tanzania kwa ajili ya uhamisho wa mshambuliaji Seleman Mwalimu mwenye umri wa miaka 19.

Wydad Yafikia Makubaliano na Singida BS Uhamisho wa Seleman Mwalimu

Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka minne utakaompeleka Wydad Casablanca kwa dau la dola 350,000 (Tshs891 milioni).

Mshahara wa Mwalimu katika klabu hiyo utakuwa ni dola 2,500 (Tshs6.3 milioni) kwa mwezi, huku pia akistahili kupata bonasi ya dola 300 (Tshs759,000) kwa kila bao atakalofunga kwenye mashindano mbalimbali.

Wydad Yafikia Makubaliano na Singida BS Uhamisho wa Seleman Mwalimu

Wydad Yafikia Makubaliano na Singida BS Uhamisho wa Seleman Mwalimu

Seleman Mwalimu ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika soka la Tanzania, sasa yuko mbioni kujiunga na Wydad, moja ya klabu kongwe na zenye mafanikio makubwa barani Afrika. Uhamisho huu ni hatua muhimu katika maendeleo ya mchezaji na pia ni ishara ya kuendelea kuvuma kwa soka la Tanzania katika anga za kimataifa.

Wachezaji na mashabiki wa Singida Black Stars watakuwa na matumaini kwamba uhamisho huu utaendelea kuboresha mchezaji na klabu yake katika soko la kimataifa.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *