Viingilio vya Mechi ya Simba dhidi ya CS Sfaxien
Viingilio vya Mechi ya Simba dhidi ya CS Sfaxien | Kuelekea mechi kubwa inayosubiriwa na mashabiki wa Simba SC, uongozi wa klabu hiyo umetoa tangazo rasmi kuhusu viingilio kwa ajili ya mashabiki watakaofurika uwanjani.
Viingilio vya Mechi ya Simba dhidi ya CS Sfaxien
Kupitia msemaji wa klabu, Ahmed Ally, viingilio hivi vimepunguzwa ili kuwahamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa timu yao sapoti kubwa.
Viingilio Vilivyopunguzwa
Haya hapa ni viwango vya viingilio vilivyotangazwa:
- Tanzanite: Tsh. 250,000
- Platinum: Tsh. 150,000
- VIP A: Tsh. 30,000 (ilipungua kutoka Tsh. 50,000)
- VIP B: Tsh. 20,000 (ilipungua kutoka Tsh. 30,000)
- VIP C: Tsh. 10,000 (ilipungua kutoka Tsh. 15,000)
- Machungwa: Tsh. 5,000 (ilipungua kutoka Tsh. 10,000)
- Mzunguko: Tsh. 3,000 (ilipungua kutoka Tsh. 5,000)
Ahmed Ally alisisitiza kuwa punguzo hili ni fursa kwa mashabiki wote wa Simba SC kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi uwanjani. Katika kauli yake, alisisitiza:
“Mwanasimba upewe nini tena? Tunaamini hakuna Mwanasimba ambaye atabaki nyumbani.”
Kupunguza viwango vya viingilio ni mkakati wa kuimarisha hamasa ya mashabiki ili waweze kutoa sapoti kubwa kwa timu yao. Ushiriki wa mashabiki uwanjani mara nyingi huwa chachu ya ushindi kwa wachezaji, hivyo Simba SC inalenga kutumia nguvu ya mashabiki wake kama silaha muhimu.
Kwa punguzo hili kubwa, mashabiki wa Simba SC wanayo kila sababu ya kujitokeza kwa wingi na kuijaza uwanja ili kuisapoti timu yao. Huu ni wakati wa kuonyesha uzalendo wa Usimba na kuhakikisha timu inapata motisha kubwa kuelekea ushindi.