FIFA Yaifungia Congo Brazzaville Kushiriki Mashindano Yote ya Soka

Filed in Michezo Bongo by on February 7, 2025 0 Comments

FIFA Yaifungia Congo Brazzaville Kushiriki Mashindano Yote ya Soka | SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limetangaza kufungiwa kwa Shirikisho la Soka la Kongo Brazzaville (FECOFOOT), ikimaanisha kuwa timu ya taifa ya Kongo na vilabu vyake vimepigwa marufuku kushiriki mashindano ya kimataifa hadi itakapotangazwa tena.

FIFA Yaifungia Congo Brazzaville Kushiriki Mashindano Yote ya Soka

Kwa mujibu wa taarifa ya FIFA, uamuzi huu umetokana na kuingiliwa kwa shughuli za shirikisho hilo na Waziri wa Michezo wa Kongo, Hugues Ngouélondélé, ambaye alivunja kamati kuu ya FECOFOOT na kuteua kamati ya muda ya usimamizi. FIFA imedai kuwa hatua hiyo inakiuka kanuni zake, hasa kifungu cha 16, ambacho kinakataza kuingiliwa na mamlaka za serikali katika shirikisho la soka la nchi yoyote.

FIFA Yaifungia Congo Brazzaville Kushiriki Mashindano Yote ya Soka

FIFA Yaifungia Congo Brazzaville Kushiriki Mashindano Yote ya Soka

Katika taarifa rasmi iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii, shirikisho la Kongo lilithibitisha kupokea notisi ya kusimamishwa kazi, ambayo itaanza kutumika rasmi kuanzia Alhamisi na kuendelea hadi ilani nyingine.

Kusimamishwa huku kunaathiri moja kwa moja kampeni ya timu ya taifa ya Kongo katika mchakato wa kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026. Ikiwa mzozo huu hautatatuliwa hivi karibuni, Kongo haitaweza kucheza mechi zake zijazo za kufuzu dhidi ya Tanzania na Zambia, zilizopangwa Machi 2025.

Aidha klabu za Kongo hazitaweza kushiriki mashindano ya kimataifa jambo ambalo linaweza kuzorotesha maendeleo ya soka la nchi hiyo. Mashabiki na wadau wa soka nchini sasa wanatarajia suluhu la haraka ili kurejesha uanachama wa FECOFOOT katika FIFA.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *