Droo ya AFCON U20 2025 Kufanyika Kesho
Droo ya AFCON U20 2025 Kufanyika Kesho | Tanzania inasubiri hatima yake. Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) litaandaa droo rasmi ya mashindano ya AFCON U-20 2025 2025 kesho, 13 Februari 2025, kuanzia 9:25 p.m. Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yamefuzu kushiriki michuano hiyo muhimu ya vijana wa U-20 ya Afrika.
Droo ya AFCON U20 2025 Kufanyika Kesho
Droo hii ndiyo itakayoamua hatima ya kila timu kwa kupanga makundi rasmi ya mashindano, yatakayotoa nafasi kwa timu za juu kutinga hatua ya mtoano. Tanzania inatarajia kupata kundi pinzani lenye nafasi ya kusonga mbele katika michuano hiyo.
Tanzania kwa mara nyingine inaingia kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 ikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri na kushindana na mataifa makubwa ya soka barani Afrika. Mashabiki wa soka wanaisubiri kwa hamu droo hii ili kujua Ngorongoro Heroes itakutana na nani katika harakati za kuwania ubingwa wa Afrika kwa vijana.
Mataifa Yaliyofuzu kwa AFCON U20 2025
Mbali na Tanzania, mataifa mengine 13 yaliyofuzu kushiriki michuano hii ni:

Droo ya AFCON U20 2025 Kufanyika Kesho
✅ Côte d’Ivoire (Wenyeji)
✅ DR Congo
✅ Misri
✅ Ghana
✅ Kenya
✅ Morocco
✅ Nigeria
✅ Senegal
✅ Sierra Leone
✅ Afrika Kusini
✅ Zambia
✅ UNIFFAC (Timu 2)
Pendekezo La Mhariri: