Yanga SC Vs KMC FC, Kocha Hamdi Aahidi Ushindi

Filed in Michezo Bongo by on February 13, 2025 0 Comments

Yanga SC Vs KMC FC, Kocha Hamdi Aahidi Ushindi | Yanga SC Yajipanga Vvizuri kwa Mchezo Dhidi ya KMC FC, Kocha Hamdi Aahidi Ushindi.

Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga SC na KMC FC utakaopigwa kesho Ijumaa, Februari 14, 2025 katika Dimba la KMC Complex, Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miloud Hamdi, amesema kuwa timu yake imejipanga vizuri kuhakikisha inapata ushindi ili kuwafurahisha mashabiki wao.

Yanga SC Vs KMC FC, Kocha Hamdi Aahidi Ushindi

Akizungumza kuelekea mchezo huo muhimu, Hamdi alisema:
“Tumejiandaa kiakili kuhakikisha tunapata ushindi na kuepuka kuwavunja moyo mashabiki wetu. Sisi sote, benchi la ufundi na wachezaji tunatamani sana kushinda mchezo huu wa kesho,” alisema Hamdi akielezea maandalizi ya timu.

Kocha huyo alikubaliana na mashabiki kwamba wanayo haki ya kutoridhika na matokeo ya baadhi ya michezo, lakini alisisitiza kuwa yeye pamoja na wachezaji wanatamani kushinda kila mchezo. Alisema kuwa mchezo wa kesho ni muhimu kwa timu na wanahitaji alama tatu.

“Ninakubaliana na mashabiki wana kila sababu ya kutoridhika kwa sababu sisi ni Klabu kubwa na mashabiki wanataka kushinda kila mchezo. Amini, hata sisi makocha na wachezaji tunataka kushinda kila mchezo. Kwa hiyo, kesho tutafanya kila tuwezalo kushinda mchezo huu kwa sababu tunahitaji alama tatu,” alisema Hamdi.

Yanga SC Vs KMC FC, Kocha Hamdi Aahidi Ushindi

Yanga SC Vs KMC FC, Kocha Hamdi Aahidi Ushindi

Kocha huyo alitoa ujumbe kwa mashabiki wa Young Africans akisisitiza kuwa timu yake inapambana kwa bidii kwa ajili yao na wachezaji wanajua majukumu yao.

“Tuko hapa kushinda mataji, hatuko hapa kwa ajili ya kazi tu, mashabiki wetu wasikate tamaa kwa sababu ya sare moja, bado tuna michezo mingi ya kucheza. Kila kitu kinawezekana, bado hatujachelewa, tuna muda, lakini lazima tufanye kila tuwezalo kushinda michezo yote ili kuwapa furaha mashabiki wetu kwa sababu wao wako pamoja nasi, na sisi pia tuko pamoja nao,” alimaliza Hamdi.

Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga SC kuendeleza rekodi yao nzuri na kupigania nafasi za juu kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huku KMC FC ikitarajiwa kutoa upinzani mkubwa. Mashabiki wa Yanga wanasubiri kwa hamu kuona kama timu yao itarudi na ushindi kutoka kwa wapinzani wao.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *