Singida Black Stars Yatoa Sababu za Kuachana na Kocha Patrick Aussems

Filed in Michezo Bongo by on February 19, 2025 0 Comments

Singida Black Stars Yatoa Sababu za Kuachana na Kocha Patrick Aussems | Klabu ya Singida Black Stars imetoa taarifa rasmi ya kuondokewa na aliyekuwa kocha wao, Patrick Aussems na kukanusha madai yaliyoenea kuwa alitimuliwa kutokana na mechi dhidi ya Yanga SC Oktoba 30, 2024 visiwani Zanzibar.

Singida Black Stars Yatoa Sababu za Kuachana na Kocha Patrick Aussems

Katika taarifa yake iliyotolewa Februari 19, 2025, uongozi wa klabu hiyo umeeleza kuwa sababu kubwa ya kumfukuza kocha huyo ni kutokuwa na sifa za kuwa kocha mkuu au kocha msaidizi kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)/Singida Black Stars Yatoa Sababu za Kuachana na Kocha Patrick Aussems.

Madai na maelezo ya klabu

Klabu ya Singida Black Stars imesema kauli zilizotolewa na Aussems baada ya kuachana na klabu hiyo mwishoni mwa 2024 ni za uongo hasa kuhusiana na kuingiliwa na uongozi katika majukumu yake ya ukocha. Klabu hiyo imesema vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti upande mmoja wa habari bila kusikiliza maelezo yake.

Sababu nyingine zilizotolewa na klabu hiyo kuachana na kocha huyo ni matokeo mabaya ya michezo mitatu aliyoiongoza huku akidai kuwa wachezaji wake wamechoka kwa kuwa hana wachezaji wa akiba wa kuchukua nafasi zao. Hata hivyo uongozi wa klabu hiyo ulisema Aussems alikataa kuwatumia baadhi ya wachezaji Kelvin Nashon, Najim Mussa na Benjamin Tanimu bila sababu za msingi jambo ambalo lilizua shaka kwa uongozi wa klabu hiyo.

Singida Black Stars Yatoa Sababu za Kuachana na Kocha Patrick Aussems

Singida Black Stars Yatoa Sababu za Kuachana na Kocha Patrick Aussems

Tuhuma kuhusu mazingira Singida

Klabu ya Singida Black Stars nayo imedai kuwa Aussems alitoa sababu nyingine zisizo za kiufundi za hali ya timu hiyo akidai kuwa Singida si sehemu nzuri kwa timu ya soka kupata mafanikio. Kwa mujibu wa klabu hiyo, kocha huyo alilalamikia mji wa Singida kukosa burudani, vilabu vya usiku, fukwe, vinywaji na maduka makubwa, hivyo akaishauri timu hiyo kuhamia miji mikubwa/Singida Black Stars Yatoa Sababu za Kuachana na Kocha Patrick Aussems.

Uongozi wa klabu hiyo uliamua kukataa ombi hilo kwa kuzingatia kuwa haiwezekani kuihama timu hiyo au kubadili jiografia ya Singida. Hatimaye, iliamuliwa kwamba Aussems aondoke na kutafuta eneo lingine ambalo lingekidhi mahitaji yake ya kibinafsi.

Matatizo ya makazi

Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa tangu Aussems ajiunge na klabu ya Singida Black Stars, amekataa malazi yaliyotolewa na klabu hiyo kwa madai kuwa anahitaji kuishi kwenye hoteli ya kifahari tu. Kocha huyo alikuwa akiishi katika hoteli ya Regency, moja ya hoteli zenye hadhi mkoani Singida, katika kipindi chote alichokuwa klabuni hapo. Hata hivyo, uongozi wa klabu ya Singida Black Stars uliona jambo hilo si endelevu kwa klabu hiyo, hivyo kuwa moja ya masuala yaliyochangia kuondoka kwake.

Klabu ya Singida Black Stars kwa sasa inaendelea na maandalizi ya mechi za ligi kuu ya NBC huku uongozi wake ukihakikisha klabu hiyo inaendelea bila matatizo ya kiufundi wala kiutawala. Endelea kufuatilia kwa taarifa zaidi kuhusu mabadiliko ndani ya Singida Black Stars na maendeleo ya timu/Singida Black Stars Yatoa Sababu za Kuachana na Kocha Patrick Aussems.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *