TANESCO Kufanya Maboresho ya Kituo cha Umeme Ubungo

Filed in Uncategorized by on February 19, 2025 0 Comments

TANESCO Kufanya Maboresho ya Kituo cha Umeme Ubungo | Maeneo ya PWANI na DAR kukosa umeme kuazia Febuary 22 hadi 28.

TANESCO Kufanya Maboresho ya Kituo cha Umeme Ubungo

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema kutakuwa na maboresho katika Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza Umeme cha Msongo wa Kilovoti 220 cha Ubungo kilichopo jijini Dar es salaam kuanzia Jumamosi, February 22 hadi February 28, 2025 ambapo wakati kazi hizo zitakapofanyika baadhi ya maeneo ya Zanzibar na Mikoa ya Dar es salaam na Pwani yataathirika kwa kukosa umeme kwa nyakati tofauti.

Taarifa ya leo Februari 19, 2025 iliyotolewa na TANESCO imesema “Hatua hii ni muhimu kwa Shirika katia kuboresha utoaji wa huduma kwa Wateja wake kufuatia ongezeko la mahitaji ya matumizi ya umeme katika maeneo ya Zanzibar na Mikoa ya Dar es Salaam, na Pwani ambalo limepelekea Kituo hicho kuzidiwa na hivyo kulazimu kufungwa kwa Mashineumba (Transformer) mpya kubwa yenye uwezo wa MVA 300ili kukidhi mahitaji ya umeme katika maeneo tajwa”

TANESCO Kufanya Maboresho ya Kituo cha Umeme Ubungo

TANESCO Kufanya Maboresho ya Kituo cha Umeme Ubungo

“Katika kipindi hicho ambacho huduma ya meme itakosekana kwa nyakati tofauti Shirika pia litakuwa likifanya matengenezo mbalimbali ya miundombinu ya umeme kwenye nmaeneo tajwa ili kuiweka miundombinu yetu kenye hali ya imara hasa kwenye kipindi hiki tunachoelekea cha msimu
wa mvua”

“Shirika linaomba radhi kwa usumbufu katika kipindi chote ambacho huduma ya umeme itakOsekana kwenye baadhi ya maeneo na litaendelea kutoa taarifa za maendeleo ya kazi hiyo mpaka kukamilika kwake”——imesema taarifa hiyo

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *