CAF Yatupilia Mbali Malalamiko ya Guinea Dhidi ya Tanzania
CAF Yatupilia Mbali Malalamiko ya Guinea Dhidi ya Tanzania
CAF Yatupilia Mbali Malalamiko ya Guinea Dhidi ya Tanzania | Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) imekataa rasmi malalamiko yaliyowasilishwa na Guinea dhidi ya Tanzania.
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Guinea lililalamikia uhalali wa mchezaji wa Taifa Stars, Mohammed Ame, kushiriki kwenye mechi kati ya Tanzania na Guinea. Katika mechi hiyo, Taifa Stars walishinda 1-0 katika mchezo uliochezwa Dar es Salaam, ushindi uliowapa tiketi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Guinea walidai kuwa mchezaji Mohammed Ame hakuwa halali kucheza kwa sababu namba yake ya jezi haikuonekana kwenye orodha ya wachezaji iliyowasilishwa kwa ajili ya mechi hiyo.
Hata hivyo, Kamati ya Nidhamu ya CAF imeamua kutupilia mbali malalamiko hayo. Matokeo ya mechi hiyo namba 143 yanabaki kama yalivyo, na Taifa Stars wanabaki na ushindi wao wa kihistoria.
Pendekezo la Mhariri: