Liverpool vs Man U, Mahasimu Wakubwa Kukutana Tena EPL Januari 5
Liverpool vs Man U, Mahasimu Wakubwa Kukutana Tena EPL Januari 5 | Ligi Kuu ya England (EPL) inaendelea leo, Januari 5, 2025, kwa mchezo wa kusisimua kati ya vinara wa ligi, Liverpool, na mahasimu wao wa jadi, Manchester United, katika dimba la Anfield.
Liverpool vs Man U, Mahasimu Wakubwa Kukutana Tena EPL Januari 5
Manchester United wanasaka ushindi wa kwanza kwenye uwanja huo tangu Januari 17, 2016, ambapo bao pekee la Wayne Rooney liliwapatia ushindi wa 1-0.
Rekodi za Hivi Karibuni za Mechi za Liverpool na Manchester United
Katika mechi sita za mwisho za EPL kati ya mahasimu hawa, Liverpool wameonyesha ubabe dhidi ya Manchester United kwa kushinda mara tatu, kutoka sare mara mbili, huku United wakipata ushindi mara moja pekee.
Mechi 6 Zilizopita (Liverpool vs Man United):
- Man United 0-3 Liverpool
- Man United 2-2 Liverpool
- Liverpool 0-0 Man United
- Liverpool 7-0 Man United
- Man United 2-1 Liverpool
- Liverpool 4-0 Man United
Ratiba ya Mechi za Leo EPL 🏴
- 17:00: Fulham vs Ipswich
- 19:30: Liverpool vs Manchester United
Liverpool wakiwa nyumbani, wana matumaini ya kuendeleza utawala wao dhidi ya Manchester United. Wakati huo huo, Mashetani Wekundu wanatarajia kufuta ukame wa ushindi katika Anfield na kuimarisha nafasi yao kwenye msimamo wa EPL.
Pendekezo La Mhariri: