Chama Aarejea Mazoezini Baada ya Wiki Tatu za Kuuguza Jeraha
Chama Aarejea Mazoezini Baada ya Wiki Tatu za Kuuguza Jeraha | Clatous Chama Aarejea Mazoezini Baada ya Wiki Tatu za Kuuguza Jeraha, Ajiandaa kwa Mchezo wa Marudiano Dhidi ya Al Hilal
Chama Aarejea Mazoezini Baada ya Wiki Tatu za Kuuguza Jeraha
Nyota wa Yanga SC, Clatous Chama, amerejea mazoezini baada ya kukosekana kwa muda wa wiki tatu akitibiwa jeraha la mkono alilopata katika mchezo dhidi ya TP Mazembe tarehe 14 Desemba 2024. Chama, ambaye alikosa mechi kadhaa za muhimu za timu yake kutokana na jeraha hilo, sasa amekuwa katika hali nzuri na tayari kwa kurudi uwanjani.
Mwamba huyo wa Lusaka anajiandaa kwa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga SC na Al Hilal kutoka Sudan, utakaopigwa Januari 12, 2025, katika dimba la Stade de la Capitale. Huu ni mchezo muhimu kwa Wananchi ambao wanahitaji ushindi ili kuongeza matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo ya kimataifa, ambapo Al Hilal wanashikilia nafasi ya juu kwenye kundi A.
Chama, ambaye ni mchezaji muhimu kwa Yanga SC, anatarajiwa kuongeza nguvu kwa timu katika mchezo huu mkubwa, huku akifanya mazoezi ya hali ya juu ili kuwa tayari kwa changamoto hiyo dhidi ya vinara wa kundi A.
Pendekezo la Mhariri: