Azam Yamaliza Usajili wa Beki Zouzou Landry Kutoka Ivory Coast
Azam Yamaliza Usajili wa Beki Zouzou Landry Kutoka Ivory Coast
USAJILI: Azam Yamaliza Usajili wa Beki Zouzou Landry Kutoka Ivory Coast | Klabu ya Azam FC imekamilisha usajili wa beki mpya, Zouzou Landry, kutoka klabu ya AFAD Djekanou ya Ivory Coast.
Zouzou, mwenye umri wa miaka 23, ambaye anajua kucheza nafasi za beki ya kati (LCB) na beki ya kushoto (LB), amesaini mkataba wa miaka minne na Azam FC, ambayo itamfanya ajiunge na timu hiyo hadi mwaka 2028.