AmaZulu Yaonyesha Nia ya Kumsajili Kibu Denis
AmaZulu Yaonyesha Nia ya Kumsajili Kibu Denis | AmaZulu wanaonyesha kumtaka mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Denis
AmaZulu Yaonyesha Nia ya Kumsajili Kibu Denis
Klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, AmaZulu FC, imetuma ofa kwa Simba SC kumsajili mshambuliaji wake, Kibu Denis (26). AmaZulu limesema limefanya mazungumzo na Wekundu hao wa Msimbazi kuhusu usajili wa mchezaji huyo ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
AmaZulu FC inayonolewa na kocha Pablo Franco Martin aliyekuwa kocha wa Simba SC kuanzia 2021 hadi 2022 inapania kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kumsajili Kibu Denis. Kocha Franco anatarajia kumtumia Kibu kuimarisha kiwango cha timu hiyo, hasa kutokana na changamoto zinazowakabili msimu huu.
Kwa sasa AmaZulu wanashika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini, wakiwa na pointi 9 katika michezo 9 waliyocheza. Msimu uliopita, klabu hiyo ilimaliza nafasi ya 11 ikiwa na pointi 36 katika michezo 30 iliyocheza. Licha ya nafasi yao ya chini, AmaZulu wana matumaini ya kuboresha kiwango chao na kupata matokeo bora.
Kibu Denis ambaye amekuwa akifanya vyema katika klabu ya Simba SC anatarajiwa kuchangia timu inayopigania kupata matokeo ya Ligi Kuu Afrika Kusini. Ofa ya AmaZulu kwa Kibu inatoa fursa nzuri kwa mchezaji huyo kuendeleza maendeleo yake katika soka la kimataifa.
Pendekezo La Mhariri: