Kocha Fadlu Amtaka Kiungo Mkabaji Moussa Conte wa CS Sfaxien

Filed in Michezo Bongo by on January 9, 2025 0 Comments

Kocha Fadlu Amtaka Kiungo Mkabaji Moussa Conte wa CS Sfaxien | Taarifa za ndani kutoka Simba SC zimeeleza kuwa kocha Fadlu Davids anavutiwa sana na uwezo wa kiungo mshambuliaji wa CS Sfaxien Balla Moussa Conte na anajipanga kumleta katika timu yake.

Kocha Fadlu Amtaka Kiungo Mkabaji Moussa Conte wa CS Sfaxien

Chanzo cha ndani kinadai kuwa baada ya mechi ya kwanza, kocha Fadlu alionyesha zaidi katika mechi ya pili ambapo Conte alicheza dakika zote tisini kwa kiwango kizuri sana, jambo ambalo lilimvutia kocha huyo.

Baada ya mechi ya pili iliyofanyika Tunisia mwishoni mwa wiki iliyopita, kocha Fadlu alimuamuru kipa wa Simba, Moussa Camara mwenye asili ya nchi moja na Conte kutoka Guinea kuzungumza na kiungo huyo.

Kocha Fadlu Amtaka Kiungo Mkabaji Moussa Conte wa CS Sfaxien

Kocha Fadlu Amtaka Kiungo Mkabaji Moussa Conte wa CS Sfaxien

Balla Moussa Conte aliyezaliwa Kamsar, Guinea, anasifika kwa uwezo wake wa kucheza kama kiungo wa ulinzi, lakini pia anaweza kucheza kama kiungo mkabaji. Alizaliwa Aprili 15, 2004 akiwa na umri wa miaka 20, Conte amekuwa mchezaji muhimu wa timu ya CS Sfaxien, ambayo alijiunga nayo Februari 1, 2023. Alipata mafunzo yake ya soka katika Chuo cha La Louvia Center nchini Guinea.

Kwa uwezo wake wa kukaba na kupiga pasi za uhakika, Conte ameonyesha kiwango cha juu na Simba SC wanaonekana kufuatilia mipango yao ya kumng’oa katika klabu yake ya sasa. Hii ni hatua nyingine kwa Simba katika kujenga timu imara na kuimarisha safu ya kiungo.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *