Yanga Yainasa Saini ya Winga Jonathan Ikangalombo
Yanga Yainasa Saini ya Winga Jonathan Ikangalombo
USAJILI Yanga Yainasa Saini ya Winga Jonathan Ikangalombo | Baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati ya Yanga na klabu ya Vita Club, hatimaye Yanga wamefanikiwa kumsajili winga Jonathan Ikangalombo Kapela (22) kwa mkataba wa miaka miwili.
Rais wa Vita Club, Amadou Diaby, amekubali kumuachia winga huyo mwenye uwezo mkubwa, na hivyo kuruhusu kuhamia kwa mchezaji huyo wa kiwango cha juu.
Ikangalombo, ambaye anajulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kutumia mguu wa kulia, tayari amewasili mjini ili kukamilisha taratibu zote za usajili. Muda wowote kuanzia sasa, winga huyo anatarajiwa kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa Yanga, ambapo ataanza rasmi safari yake kwenye timu hiyo ya jangwani.
Huu ni usajili mwingine muhimu kwa Yanga, inayolenga kuimarisha safu ya ushambuliaji wake na kuongeza ufanisi katika michuano mbalimbali ya msimu huu. Ikangalombo Kapela anatarajiwa kuleta mchango mkubwa katika timu ya Yanga, akiwasaidia kutimiza malengo yao katika ligi kuu na michuano ya kimataifa.
Pendekezo La Mhariri: