Robert Matano Atangazwa Kocha Mkuu wa Fountain Gate
Robert Matano Atangazwa Kocha Mkuu wa Fountain Gate | Kocha wa zamani wa Sofapaka ya Kenya Robert Matano ametangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa klabu ya Fountain Gate FC yenye maskani yake mjini Babati nchini Tanzania.
Matano raia wa Kenya na mmoja wa makocha waliofanya vizuri katika soka la Afrika Mashariki anachukua nafasi ya Mohamed Muya aliyetimuliwa hivi karibuni kwa matokeo yasiyoridhisha.
Robert Matano Atangazwa Kocha Mkuu wa Fountain Gate
Matano ana historia ya mafanikio katika soka la Kenya, akiwa ameshinda mataji manne ya Ligi Kuu ya Kenya. Alishinda mataji matatu kati ya hayo akiwa na Tusker FC, huku jingine akiwa na Sofapaka FC. Uzoefu wake mkubwa na mafanikio haya yanatarajiwa kuleta mabadiliko chanya ndani ya Fountain Gate FC.
Katika jukumu lake jipya, Matano ataungwa mkono na Amri Said, ambaye pia ni mkufunzi wa Fountain Gate FC. Ushirikiano huu unalenga kuboresha matokeo ya timu na kuimarisha nafasi ya Fountain Gate katika mashindano ya ndani na kimataifa.
Matano anakabiliwa na changamoto ya kuirejesha Fountain Gate FC katika njia za ushindi huku akiboresha timu ili kufikia malengo ya muda mfupi na mrefu ya klabu. Aidha, uzoefu wao unatarajiwa kuwapa wachezaji maandalizi ya kiufundi na kiakili ili kuboresha ujuzi wao uwanjani.
Pendekezo La Mhariri: