Zanzibar Heroes Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025

Filed in Michezo Bongo by on January 11, 2025 0 Comments

Zanzibar Heroes Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025

Zanzibar Heroes Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025 | Michuano ya Kombe la Mapinduzi 2025 imeendelea kwa msisimko, huku Zanzibar Heroes ikijihakikishia nafasi ya kucheza fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Harambee Stars ya Kenya.

Mchezo huo wa nusu fainali, uliofanyika Januari 10, 2025, ulikuwa wa vuta nikuvute na ulishuhudia idadi kubwa ya kadi zikionyeshwa na mwamuzi.

Zanzibar Heroes Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025

Zanzibar Heroes Yatinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi 2025

Matokeo ya Mchezo

  • FT: Kenya 0-1 Zanzibar Heroes
  • Bao: Ali Juma ‘Inzangi’ dakika ya 90+4

Bao hilo la dakika za majeruhi lilifungwa na Ali Juma maarufu kama ‘Inzangi,’ ambaye alitokea shujaa wa Zanzibar Heroes kwa kuipa timu yake tiketi ya fainali.

Mchezo huu ulisimama kama mmoja wa mechi zenye ushindani mkubwa, huku mwamuzi akitoa kadi 10 kwa wachezaji wa timu zote mbili. Kadi nyekundu mbili zilitolewa pamoja na kadi za njano 8, hali iliyodhihirisha ukali wa pambano hilo.

Ratiba ya Fainali

Zanzibar Heroes sasa itaingia fainali kukutana na Burkina Faso, timu ambayo pia imeonyesha uwezo mkubwa katika michuano hii. Mchezo wa fainali unatarajiwa kupigwa Januari 13, 2025, kwenye Uwanja wa Gombani, na unatarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wa soka kutoka kila kona ya Zanzibar na kwingineko.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *