Simba Yafuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF
Simba Yafuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF
Simba Yafuzu Robo Fainali Kombe la Shirikisho CAF | Wawakilishi wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho Afrika, Simba Sc imetinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo kufuatia sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji Bravos do Marquis ya Angola katika dimba la Estádio Da Tundavala kwenye mchezo wa raundi ya tano wa Kundi A.
Bravos 🇦🇴 1-1 🇹🇿 Simba SC
⚽ 13’ Abednego
⚽ 69’ Ateba
FT: CS Constantine 🇩🇿 2-0 🇹🇳 CS Sfaxien
MSIMAMO KUNDI A
1. 🇩🇿 Constantine— mechi 5—pointi 12
2. 🇹🇿 Simba Sc — mechi 5—pointi 10
3. 3. 🇦🇴 Bravos — mechi 5—pointi 7
4. 🇹🇳 CS Sfaxien — mechi 5—pointi 🅾️
Kwenye CAF timu zikilingana pointi Sheria ya ‘tie breaker’ inaangalia matokeo baina ya timu hizo (head to head) kwanza.
Kwa maana hiyo kwa kuwa Simba Sc iliifunga Bravos na kutoka nayo sare kwenye marudiano, hivyo tayari ameondoshwa kwenye michuano hata kama Simba Sc itapoteza kwa idadi yoyote ya magoli kwenye mechi ya mwisho.
Pendekezo La Mhariri: