Yanga Yaongeza Matumaini ya Kufuzu Robo Fainali ya CAFCL
Yanga Yaongeza Matumaini ya Kufuzu Robo Fainali ya CAFCL | Yanga SC Yashinda 1-0 Dhidi ya Al Hilal na Kuongeza Matumaini ya Kufuzu Robo Fainali ya CAFCL
Yanga Yaongeza Matumaini ya Kufuzu Robo Fainali ya CAFCL
Yanga SC imeendelea kuweka matumaini yao ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) hai, baada ya kushinda 1-0 dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan katika mchezo wa Kundi A uliofanyika katika dimba la Cheikha Ouldi Boidiya, Mauritania.
Ushindi huu ulitokana na bao la mapema la Aziz Ki katika dakika ya 7, ambalo lilitosha kuwaondoa Al Hilal na kuweka Yanga kwenye nafasi nzuri ya kufuzu.
Yanga SC sasa wanahitaji ushindi wowote katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya MC Alger ya Algeria, utakaochezwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, ili kufuzu hatua ya robo fainali. Huu utakuwa ni mchezo wa kuamua kama Yanga wataendelea kwenye michuano hii ya kimataifa au la.
Matokeo ya Mchezo:
FT: Al Hilal πΈπ© 0-1 πΉπΏ Yanga SC
πΉπΏ 7β Aziz Ki
MSIMAMO KUNDI A CAFCL
- πΈπ© Al Hilal β Mechi 5 β Pointi 10
- π©πΏ MC Alger β Mechi 5 β Pointi 8
- πΉπΏ Yanga SC β Mechi 5 β Pointi 7
- π¨π© Mazembe β Mechi 5 β Pointi 2
Yanga SC sasa wanajiandaa kwa mchezo wa mwisho wa kundi, wakilenga kumaliza katika nafasi ya pili au tatu ili kuendelea katika hatua inayofuata ya michuano hii ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Pendekezo La Mhariri: