Jinsi ya Kushiriki Kampeni ya Simba, TUNAWAJIBIKA PAMOJA

Filed in Michezo Bongo by on January 15, 2025 0 Comments

Jinsi ya Kushiriki Kampeni ya Simba, TUNAWAJIBIKA PAMOJA | Klabu ya Simba Sc imezindua rasmi kampeni iliyopewa jina la TUNAWAJIBIKA PAMOJA kwa ajili ya mashabiki wake kuchangia kiasi cha fedha ili kulipa faini Tsh Milioni 100 waliyotozwa na Shirikisho la soka Afrika (CAF) kufuatia mashabiki wake kufanya fujo kwenye mchezo dhidi ya CS Sfaxien ambapo klabu hiyo imetoa akaunti za kuchangia kiasi hicho.

“Tumekuja na kampeni maalumu ambayo hii imeombwa na amshabiki wenyewe wakitaka kuwajibika baada ya kufanya makosa yale. Tumewaletea mfumo wa kuchangia ili kitakachopatikana twende tukalipe faini na Simba Sports Club ibaki salama. Kampeni hiyo tumeipa jina la TUNAWAJIBIKA PAMOJA.” — Ahmed Ally, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Sc,

Jinsi ya Kushiriki Kampeni ya Simba, TUNAWAJIBIKA PAMOJA

“Natoa rai kwa Wanasimba, asijekutokea Mwanasimba wa kuchangisha kwamba kikifika kiasi fulani tutapeleka ofisini. Kila Mwanasimba atume fedha yake moja kwa moja kwenye namba ya ofisi ambayo imetolewa”

“Zoezi letu tumeliweka kwa muda sio kwa kiwango kwahiyo kama ikifika milioni 100 na muda bado tutawaachia. Wanasimba wanapaswa kuonyesha nguvu yao, wanapaswa kusimama na timu yao”— Ahmed Ally.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *