Inaki Williams Afanyiwa Upasuaji, Atolewa Kipande cha Glasi Mguuni
Inaki Williams Afanyiwa Upasuaji, Atolewa Kipande cha Glasi Mguuni | Straika wa timu ya Athletic Bilbao, Inaki Williams, amecheza soka kwa miaka miwili akiwa na kipande cha glasi mguuni mwake, baada ya kujeruhiwa kwenye ajali aliyopata miaka miwili iliyopita.
Inaki Williams Afanyiwa Upasuaji, Atolewa Kipande cha Glasi Mguuni
Meneja wa timu hiyo, Ernesto Valverde, alifafanua kuwa Williams alipata ajali ambapo kioo kilipasuka na akakanyaga kipande cha glasi bila kujua.
Baada ya majeraha hayo, Williams alionekana kupona na kuendelea kucheza, lakini katika miezi ya hivi karibuni, tatizo hilo liliibuka tena na kuanza kumtesa. Hali hiyo iliwalazimu kufanya uchunguzi zaidi, ambapo waligundua kuwa kipande cha glasi kilikuwa kimesalia mguuni mwake, likiwa na ukubwa wa sentimeta 2 na lilikuwa karibu na mfupa au tendon.
Valverde alisema, “Tulifanya uchunguzi baada ya fainali ya Copa del Rey na tukagundua kuwa alikuwa bado na kipande cha chupa mguuni. Walipomshona kwa mara ya kwanza, waliacha chupa mle ndani. Kwa kuongeza, sio kipande kidogo, ni kama sentimeta 2. Ilikuwa karibu na mfupa au tendon, lakini ilitubidi kuiondoa. Ukweli ni kwamba mimi na daktari tulikuwa tunacheka kwa sababu hatukuamini.”
Williams alifanyiwa upasuaji ili kuondoa kipande hicho cha glasi, na sasa anatarajiwa kurejea uwanjani baada ya kupona. Huu ni mfano mwingine wa uvumilivu wa mchezaji ambaye aliendelea kupigana licha ya maumivu na changamoto alizokutana nazo.
Pendekezo La Mhariri: