Yondani Ateuliwa Kuwa Nahodha Mkuu Kengold FC
Yondani Ateuliwa Kuwa Nahodha Mkuu Kengold FC | Kelvin Yondani ameteuliwa kuwa nahodha mkuu wa Kengold FC huku timu hiyo ikijitahidi kujinasua kutoka mkiani mwa Ligi Kuu ya NBC.
Yondani Ateuliwa Kuwa Nahodha Mkuu Kengold FC
Yondani ambaye ni mchezaji mzoefu atakuwa na kibarua cha kuinoa timu hii ambayo kwa sasa ipo nafasi ya mwisho (16) kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 6 katika mechi 16 ilizocheza hadi sasa.
Kengold FC inakabiliwa na changamoto kubwa kwani ni timu inayopigania kubaki Ligi Kuu na uteuzi wa Yondani kuwa nahodha mkuu unalenga kuongeza ari na nguvu katika kikosi cha timu hiyo. Yondani atatumia uzoefu wake wa kimataifa na uongozi uwanjani kuwasaidia wachezaji wenzake kujitahidi kupata matokeo bora ili kuibuka na janga hili.
Kengold FC kwa sasa inahitaji kushinda mechi nyingi ili kuepuka kushuka daraja, na matarajio ni kwamba kwa kuwa na nahodha mzoefu kama Yondani, timu hiyo itakuwa na msukumo mpya wa kuhakikisha inapata matokeo bora katika mechi zijazo.
Pendekezo La Mhariri: