Singida Black Stars Kumezidi Kuchangamka
Singida Black Stars Kumezidi Kuchangamka | Singida Black Stars Yatoa Siku 14 kwa Gor Mahia Kulipa USD 40,000 ya Rooney Onyango, Singida Black Stars Wamaliza Kambi Arusha, Wajipanga kwa Mechi Dhidi ya Kagera Sugar Februari 7.
Singida Black Stars Kumezidi Kuchangamka
Singida Black Stars yaipa Gor Mahia siku 14 kulipa USD 40,000
Klabu ya Singida Black Stars ya Tanzania 🇹🇿 wameandika notisi ya siku 14 kwa klabu ya Gor Mahia ya Kenya 🇰🇪 kuhakikisha wamerudisha kiasi cha USD 40,000 (sawa na Tshs 101.8 milioni) ambazo walilipwa kama ada ya usajili wa mchezaji Rooney. Onyango, beki wa kulia.
Mchezaji huyo aligoma kujiunga na Singida licha ya makubaliano kati ya klabu hizo mbili. Singida sasa wanataka kurudishiwa fedha hizo baada ya dili la uhamisho wa beki huyo kushindikana.
Singida Black Stars wamaliza kambi ya Arusha na kuanza safari ya kurejea Singida
Timu ya Singida Black Stars imemaliza kambi yake ya wiki tatu jijini Arusha. Maandalizi haya yalifanywa kujiandaa na mechi zao zijazo.
Leo Januari 30, 2025 timu imeanza safari ya kurejea Singida kuendelea na maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC 🇹🇿 dhidi ya Kagera Sugar. Mechi hii imepangwa kuchezwa Februari 7 kwenye Uwanja wa CCM Liti.
Pendekezo La Mhariri: