CAF Yaruhusu Mchezaji Kucheza Klabu Mbili Katika Msimu Mmoja
CAF Yaruhusu Mchezaji Kucheza Klabu Mbili Katika Msimu Mmoja Kwenye Mashindano yote ya CAF | CAF Yabadili Kanuni za Usajili Katikati ya Mashindano ya Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho.
CAF Yaruhusu Mchezaji Kucheza Klabu Mbili Katika Msimu Mmoja
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limefanya mabadiliko muhimu ya kanuni za usajili wa wachezaji kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika mabadiliko hayo, klabu za soka sasa zitaweza kusajili mchezaji aliyeshiriki mashindano hayo na klabu nyingine ndani ya msimu huo wa soka. Hii ina maana kwamba mchezaji anaweza kuanza msimu akichezea klabu moja katika mashindano ya CAF na kisha kuhamia klabu nyingine inayoshiriki mashindano hayo na bado anaweza kucheza.
Kwa hatua hiyo, CAF itafuata mfumo wa usajili unaotumiwa na UEFA Champions League na UEFA Europa League, ambapo wachezaji wanaweza kushiriki mashindano ya vilabu vya Ulaya hata baada ya kuhama kutoka klabu moja kwenda nyingine.
Mabadiliko haya yanatarajiwa kuleta urahisi kwa vilabu na wachezaji, huku pia yakiongeza ushindani katika mashindano ya CAF kwa sababu vilabu vikubwa sasa vinaweza kuimarisha vikosi vyao hata katikati ya msimu.
Pendekezo La Mhariri: