Barcelona Yampa Gavi Mkataba Mpya Mpaka 2030
Barcelona Yampa Gavi Mkataba Mpya Mpaka 2030 | Barcelona wanaendelea kuimarisha mustakabali wa wachezaji wao chipukizi kwa mipango ya muda mrefu na sasa wanakaribia kumsajili kiungo Gavi kwa mkataba mpya utakaomweka klabuni hapo hadi 2030.
Hatua hiyo imekuja saa chache baada ya Barcelona kumsaini Pedri kwa kandarasi ya muda mrefu hadi Juni 2030, kuonyesha nia ya klabu hiyo kuhakikisha vipaji muhimu vinasalia Nou Camp kwa miaka ijayo.
Mkataba wa Gavi unasemekana kuwa na kipengele cha kuachiliwa kwa dola za Marekani bilioni moja, sawa na Tsh. trilioni 2.5, ikiwa ni hatua ya kuhakikisha klabu nyingine haziwezi kumpokonya kiungo huyo kirahisi.
Mpango huu wa Barcelona ni sehemu ya mkakati wa kujenga kizazi kipya cha wachezaji bora, huku wakiwahakikishia nyota wao wakubwa kubaki klabuni hapo kwa muda mrefu kuwania mataji makubwa ya Ulaya
Pendekezo La Mhariri: