Ajali ya Basi la Dodoma Jiji Yakumba Timu Asubuhi Hii
Ajali ya Basi la Dodoma Jiji Yakumba Timu Asubuhi Hii
Ajali ya Basi la Dodoma Jiji Yakumba Timu Asubuhi Hii | Basi la timu ya Dodoma Jiji FC limepata ajali mapema asubuhi ya leo katika maeneo ya Nangurukuru kuelekea Somanga, mkoani Lindi. Timu hiyo ilikuwa safarini ikitokea mjini Ruangwa, ambapo jana walishiriki mechi ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Namungo FC.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wachezaji wa Dodoma Jiji FC wamefanikiwa kunusurika na ajali hiyo bila kupata madhara makubwa. Hata hivyo, taarifa zinasema baadhi ya mafunzo wamepata majeraha madogo.

Ajali ya Basi la Dodoma Jiji Yakumba Timu Asubuhi Hii
Ajali hii inakuja wakati timu nyingi zikihangaika na changamoto za usafiri zinazokabili michezo ya Ligi Kuu ya NBC, hasa kwa timu zinazotembelea maeneo mbalimbali. Hali ya usalama barabarani inabakia kuwa suala la muhimu, huku timu zikihitajika muda mrefu kwa ajili ya mechi za ligi.
Mashabiki wa Dodoma Jiji FC pamoja na wadau wa michezo wanatarajia taarifa zaidi kuhusu hali ya afya ya wachezaji na maendeleo ya timu baada ya ajali hii.
Pendekezo La Mhariri: