Al Nassr Mbioni Kukamilisha Usajili wa Victor Boniface
Al Nassr Mbioni Kukamilisha Usajili wa Victor Boniface | Klabu ya Al Nassr FC inaripotiwa kuwa karibu kukamilisha usajili wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Bayer 04 Leverkusen, Victor Boniface, kwa jumla ya ada inayokadiriwa kufikia £55 milioni.
Al Nassr Mbioni Kukamilisha Usajili wa Victor Boniface
Mshambuliaji huyo kutoka Nigeria amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu, jambo lililovutia vilabu kadhaa, lakini Al Nassr wameonekana kuwa na dhamira thabiti ya kumsajili ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji.
Ushindani wa ligi na ndoto ya kutwaa ubingwa zimekuwa changamoto kubwa kwa Al Nassr. Nyota wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo (CR7), anaonekana kuwa na shauku ya kuisaidia klabu hiyo kutwaa taji la ligi kabla ya kuhitimisha safari yake ndani ya klabu hiyo. Usajili wa Boniface unatarajiwa kuleta nguvu mpya kwa kikosi hicho ili kufanikisha ndoto ya kuleta kombe nyumbani.
Iwapo dili hili litakamilika, Boniface atakuwa miongoni mwa wachezaji ghali zaidi kuwahi kusajiliwa na klabu kutoka Mashariki ya Kati. Mchango wake unatarajiwa kuongeza kasi ya ushindani wa Al Nassr na kuwapa matumaini ya mafanikio ya muda mfupi na mrefu.
Pendekezo La Mhariri: