Alaa Meskini Aondoka Yanga SC, Ajiunga na FAR Rabat
Alaa Meskini Aondoka Yanga SC, Ajiunga na FAR Rabat | KOCHA wa makipa wa Yanga SC, Mmorocco Alaa Meskini, ameachana rasmi na klabu hiyo na kujiunga na FAR Rabat ya nchini kwao. Uamuzi wake wa kuondoka Yanga SC umekuja baada ya baba yake kupata msiba mzito uliomfanya aamue kurejea nyumbani ili kuwa karibu na familia yake.
Alaa Meskini ambaye alikuwa kiungo muhimu wa kikosi cha ufundi cha Yanga SC, sasa ameaga rasmi na kuondoka jijini Dar es Salaam na vitu vyake vyote. Kuondoka kwake kumekuja wakati Yanga SC ikiendelea na kampeni zake katika michuano mbalimbali, ikiwamo Ligi Kuu ya NBC na michuano ya kimataifa.
Kuondoka kwa Meskini kunaweza kuleta changamoto kwa makipa wa Yanga kwani amekuwa na mchango mkubwa katika mazoezi ya makipa wa timu hiyo. Klabu hiyo inatarajiwa kupata haraka mbadala wa kuziba pengo lake na kuhakikisha timu inabaki imara.

Alaa Meskini Aondoka Yanga SC, Ajiunga na FAR Rabat
Kwa sasa mashabiki wa Yanga SC wanamsindikiza kwa heshima kocha huyo na kumtakia kila la heri katika safari yake mpya ya FAR Rabat. Bado haijafahamika iwapo Yanga SC itatafuta kocha mpya wa makipa au itatumia mbinu nyingine kuhakikisha nafasi hiyo inasimamiwa ipasavyo.
Pendekezo La Mhariri: