Aziz Ki Aandika Hat-Trick, Yanga Yaichapa KMC FC 6-1
Aziz Ki Aandika Hat-Trick, Yanga Yaichapa KMC FC 6-1 | Kiungo wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki amethibitisha ubora wake kwa kufunga hat-trick katika ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya KMC FC Uwanja wa KMC Complex. Hii ni hat-trick yake ya pili msimu wa 2024/25, na ya pili kwa Yanga SC msimu huu, baada ya ile ya kwanza kufungwa na Prince Dube.
Aziz Ki Aandika Hat-Trick, Yanga Yaichapa KMC FC 6-1
Matokeo ya mechi: KMC FC 1-6 Yanga SC
⚽ 11’ – Prince Dube
⚽ 18’ – Stephane Aziz Ki (P)
⚽ 49’ – Stephane Aziz Ki
⚽ 56’ – Stephane Aziz Ki (P) (Hat-trick)
⚽ 90’ – Maxi
⚽ 90+4’ – Mwenda
⚽ 52’ – Redemptus (KMC)
Kwa matokeo hayo, Yanga SC wameendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC wakiwa na pointi 49 baada ya mechi 19, wakizidiwa na Simba SC wanaoshika nafasi ya pili kwa mechi moja.

Aziz Ki Aandika Hat-Trick, Yanga Yaichapa KMC FC 6-1
Aziz Ki akiendelea kung’ara
Hat-trick ya Aziz Ki inathibitisha ubora wake msimu huu, na anabaki kuwa mhimili wa Yanga SC katika safu ya ushambuliaji. Mbali na kufunga mabao yote matatu, amekuwa na mchango mkubwa kwa kutengeneza nafasi za kufunga kwa timu yake.
Rekodi ya Yanga SC ya kufunga hat-trick msimu huu
1️⃣ Prince Dube: hat-trick yake ya kwanza msimu huu
2️⃣ Stephane Aziz Ki: hat-trick yake ya pili msimu huu
Yanga SC wanaendelea kuonyesha nguvu katika mbio za kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya NBC, huku safu yao ya ushambuliaji ikitamba msimu huu. Mashabiki wa Wananchi wanatarajia kuendelea kuona mambo mazuri kutoka kwa nyota wao katika mechi zijazo.
Pendekezo La Mhariri: