Barcelona Yatinga Fainali kwa Ushindi wa 2-0 Dhidi ya Athletic Club
Barcelona Yatinga Fainali kwa Ushindi wa 2-0 Dhidi ya Athletic Club | Klabu ya FC Barcelona imefanikiwa kufuzu kwa fainali ya Spanish Super Cup baada ya kushinda 2-0 dhidi ya Athletic Club katika mechi iliyopigwa kwenye dimba la King Abdullah Sports City mjini Jeddah, Saudi Arabia.
Mabao ya ushindi kwa Barcelona yalifungwa na Gavi katika dakika ya 17 na Lamine Yamal katika dakika ya 52.
Kwa matokeo hayo, Barcelona inasubiri kushuhudia nani atakayekutana nao kwenye fainali – Real Madrid au Mallorca – ambao watacheza nusu fainali nyingine Alhamisi, Januari 9, 2025, kwenye uwanja huo huo wa King Abdullah Sports City.
Barca itaendelea na ndoto ya kutwaa kombe la Spanish Super Cup, huku mashabiki wakiwa na matumaini ya kuona timu yao ikionyesha ubora mkubwa katika fainali hiyo.
Pendekezo La Mhariri: