Bondia Hassan Mgaya Afariki Dunia Baada ya Pambano Jijini Dar es Salaam
Bondia Hassan Mgaya Afariki Dunia Baada ya Pambano Jijini Dar es Salaam | Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Hassan Mgaya, amefariki dunia usiku wa Jumapili, Desemba 28, 2024. Kifo chake kimetokea muda mfupi baada ya kupewa rufaa ya kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka Hospitali ya Mwananyamala.
Bondia Hassan Mgaya Afariki Dunia Baada ya Pambano Jijini Dar es Salaam
Taarifa zinasema kuwa Mgaya alizidiwa baada ya kushiriki pambano la ngumi lililofanyika Jumamosi, Desemba 27, 2024, kwenye Ukumbi wa Dunia Ndogo, Tandale jijini Dar es Salaam. Katika pambano hilo, alishindana na bondia Paul Elias ambapo aliumia vibaya baada ya kupigwa ngumi nyingi za kichwa katika raundi ya tano. Tukio hilo lilisababisha kuanguka, kung’ata ulimi, na kupoteza fahamu.
Baada ya kuanguka, alihudumiwa huduma ya kwanza na kufanikiwa kurejea katika hali yake ya kawaida. Hata hivyo, hali yake ilianza kubadilika asubuhi ya Jumapili, akakimbizwa katika Hospitali ya Palestina, kisha kuhamishiwa Hospitali ya Mwananyamala kabla ya kupewa rufaa ya kwenda Muhimbili.
Mweka Hazina wa Chama cha Mabondia, Cosmas Cheka, amethibitisha kifo cha Mgaya akisema kilitokea wakati wakiwa njiani kuelekea Muhimbili kutokana na kuzidiwa zaidi.
Hassan Mgaya ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania.
Pendekezo la Mhariri: