CAF Yaongeza Muda wa Usajili kwa Timu za CAF Interclub
CAF Yaongeza Muda wa Usajili kwa Timu za CAF Interclub | SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza kuongeza muda wa usajili kwa timu zinazoshiriki mashindano ya CAF baina ya vilabu na Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA.
CAF Yaongeza Muda wa Usajili kwa Timu za CAF Interclub
Mabadiliko hayo yanaziathiri timu ambazo zimefuzu kwa robo fainali ya michuano ya CAF baina ya klabu, pamoja na timu zinazoshiriki Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA mwaka huu.
Tarehe ya mwisho ya usajili ilipangwa kufungwa Januari 31, 2025, lakini sasa imeongezwa hadi Februari 28, 2025. Uamuzi huo unalenga kuzipa timu fursa ya kufanya mabadiliko makubwa kwenye orodha zao kabla ya kuendelea na michuano hiyo muhimu.
Hii ni hatua muhimu kwani itaruhusu baadhi ya timu kurekebisha orodha zao kwa kuongeza wachezaji wapya au kufanya mabadiliko mengine muhimu, hasa kutokana na changamoto za kimataifa na ushindani mkali wa michuano hiyo.
CAF pia inaangalia njia za kuhakikisha kuwa timu za Afrika zina nafasi nzuri ya kushiriki mashindano ya kimataifa, na kuongeza muda wa usajili ni sehemu ya kuhakikisha hilo linafanyika.
Pendekezo La Mhariri: