Che Malone Awaomba Radhi Wanasimba
Che Malone Awaomba Radhi Wanasimba | Beki kitasa wa Simba Sc, Che Fondoh Malone (25) almaarufu ‘Ukuta wa Yeriko’ raia wa Cameroon ameomba radhi kwa kosa alilofanya jana kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika lililoigharimu timu hiyo kuruhusu bao la mapema dhidi ya Bravos do Marquis ya Angola.
Che Malone Awaomba Radhi Wanasimba
“Napenda kuomba radhi kwa familia nzima ya Simba Sc kwa kuwagharimu sana kwenye mechi mbili. Nawajibika kikamilifu kwa makosa yangu na kuahidi kufanya kazi kwa bidii zaidi ili kufanya vizuri zaidi katika siku zijazo.
Samahani sana, Asante Simba,
Asanteni mashabiki kwa kunitia moyo kila mara licha ya kuwakatishwa tamaa.”—ameandika Che Malone kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.
Hii ni mara ya pili kwenye kombe la Shirikisho kwa Che Malone kufanya ‘blunder’ iliyoigharimu timu kuruhusu bao baada ya ya ile ‘back pass’ mbovu kwenye mechi dhidi ya CS Sfaxien kabla ya Kibu Dennis kufunga magoli mawili na kuinusuru timu.
Katika mchezo wa jana dhidi ya Bravos, alipoteza umakini na kupiga ‘back pass’ iliyookotwa na mpinzani kabla ya Simba Sc kuruhusu bao la mapema kabla ya Lionel Ateba kusawazisha na kuinusuru timu na kipigo.
Pendekezo La Mhariri: