Droo ya Futsal AFCON 2025 kwa Wanawake Kufanyika Kesho

Filed in Michezo Bongo by on February 12, 2025 0 Comments

Droo ya Futsal AFCON 2025 kwa Wanawake Kufanyika Kesho | Tanzania itaingia kwenye kundi gumu?

Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetangaza kuwa droo rasmi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 kwa Futsal kwa Wanawake itafanyika kesho, 13 Februari 2025, kuanzia saa 8:00 mchana. Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyofuzu kushiriki mashindano hayo ya futsal, ambayo ni ya kwanza kwa wanawake kuandaliwa kwa kiwango hiki cha juu barani Afrika.

Droo hiyo itaamua makundi ya mashindano na kuonyesha njia ya kila timu kuelekea Mashindano ya Afrika ya Futsal kwa Wanawake. Tanzania inatarajiwa kuwa katika kundi lenye ushindani mkubwa, hasa kutokana na uwepo wa mataifa yenye uzoefu wa mchezo wa futsal kama Morocco, Misri na Cameroon.

Droo ya Futsal AFCON 2025 kwa Wanawake Kufanyika Kesho

Droo ya Futsal AFCON 2025 kwa Wanawake Kufanyika Kesho

Droo ya Futsal AFCON 2025 kwa Wanawake Kufanyika Kesho

Mataifa Yaliyofuzu kwa Futsal AFCON 2025 kwa Wanawake

Mbali na Tanzania, mataifa mengine yaliyofuzu kushiriki michuano hii ni:

Morocco (Wenyeji)
Angola
Cameroon
Misri
Guinea
Madagascar
Namibia
Senegal

Kwa kuwa hii ni moja ya fursa muhimu kwa soka la wanawake nchini Tanzania, Timu ya Taifa ya Wanawake ya Futsal inatarajia kuonyesha ushindani mkubwa ili kufanikisha safari yao ya kuelekea kwenye michuano hiyo ya kihistoria.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *