Feisal Salum Msimu wa Mafanikio na Kiwango Bora NBC
Feisal Salum Msimu wa Mafanikio na Kiwango Bora NBC Ligi Kuu Tanzania Bara | Feisal Salum, maarufu kama Fei Toto, anaendelea kuthibitisha ubora wake kama mmoja wa viungo mahiri katika ligi kuu ya Tanzania (NBC Premier League).
Feisal Salum Msimu wa Mafanikio na Kiwango Bora NBC
Msimu wa 2023/2024 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwake, akifunga mabao 19 na kutoa pasi za mabao (assists) 8, rekodi iliyomfanya aonekane kuwa moja ya wachezaji muhimu zaidi katika ligi hiyo.
Katika msimu uliopita, Feisal alionyesha juhudi kubwa, lakini kilele cha mafanikio kimeonekana zaidi msimu huu wa 2024/2025. Kufikia katikati ya msimu huu, Feisal tayari ametoa assists 9 na kufunga mabao 4, idadi inayozidi kiwango alichokifikisha msimu uliopita.
Ni wazi kwamba Feisal anaendelea kuimarika msimu baada ya msimu, tangu aanze kucheza kama kiungo mshambuliaji wa juu (Advanced Attacking Midfielder) chini ya kocha Nabi. Takwimu zake zinadhihirisha jinsi kiwango chake kinavyopanda kwa kasi, na mchango wake uwanjani umekuwa wa kuaminika kwa timu yake.

Feisal Salum Msimu wa Mafanikio na Kiwango Bora NBC
Thamani ya Mchezaji
Mbali na takwimu za uwanjani, thamani ya Feisal kama mchezaji pia imekuwa ikiongezeka. Katika ligi ya NBC Premier League, jina lake linatajwa miongoni mwa wachezaji wenye thamani kubwa zaidi kutokana na uwezo wake wa kuamua mechi na kuongoza timu kupitia nafasi yake ya kiungo mshambuliaji.
Feisal Salum ameendelea kujidhihirisha kuwa lulu katika soka la Tanzania. Kiwango chake na nidhamu yake ya kazi vinampa nafasi ya kuwa kiungo bora zaidi wa kizazi hiki. Kwa namna anavyoendelea, wapenzi wa soka wana kila sababu ya kutarajia makubwa zaidi kutoka kwake msimu huu na misimu ijayo/Feisal Salum Msimu wa Mafanikio na Kiwango Bora NBC.
Pendekezo La Mhariri: