Gadiel Michael Ajiunga na Singida Black Stars, Mkataba wa Miaka Miwili
Gadiel Michael Ajiunga na Singida Black Stars, Mkataba wa Miaka Miwili | Beki wa pembeni wa timu ya Taifa ya Tanzania, Gadiel Michael Kamagi amejiunga na Singida Black Stars kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini akiwa mchezaji huru.
Gadiel Michael Ajiunga na Singida Black Stars, Mkataba wa Miaka Miwili
Uhamisho huu ni mapinduzi makubwa kwa upande wa Singida kwani Gadiel anakuja na uzoefu mkubwa wa ligi ya ndani na kimataifa.
Gadiel aliyewahi kuzichezea klabu za Tanzania kama Azam FC, Yanga SC, Simba SC na Singida Fountain Gate FC, ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na amekuwa sehemu muhimu ya timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Uzoefu wake katika ligi kuu za Afrika na michuano ya kimataifa unatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Singida Black Stars inayojivunia kikosi kilichojaa wachezaji bora.
Gadiel Kamagi na hadithi yake ya mafanikio
Gadiel amekuwa mmoja wa mabeki bora wa pembeni Tanzania na ameonyesha uwezo mkubwa katika kushambulia na kuzuia. Uhamisho huu unaiongezea nguvu safu ya ulinzi ya Singida, huku klabu hiyo ikijitahidi kuwania nafasi nzuri ya kucheza Ligi Kuu ya NBC msimu huu.
Kwa mkataba huu mpya, Gadiel Michael Kamagi atapata fursa ya kuonyesha ujuzi wake katika Ligi Kuu ya NBC, huku akiisaidia klabu ya Singida Black Stars kuendeleza mafanikio na kuwania ubingwa wa ligi hiyo. Mashabiki wa Singida wana matumaini kuwa beki huyu atakuwa nguzo muhimu kwa timu yao katika michuano ijayo.
Pendekezo la Mhariri: