Heritier Imana Ajiunga na Al Mahdia ya Libya kutoka AS Vita Club
Heritier Imana Ajiunga na Al Mahdia ya Libya kutoka AS Vita Club | Winga Heritier Imana Lote mwenye umri wa miaka 23 kutoka Jamhuri ya Kongo (DRC Congo) amejiunga na klabu ya Al Mahdia ya Libya akitokea AS Vita Club.
Heritier Imana Ajiunga na Al Mahdia ya Libya kutoka AS Vita Club
Lote ambaye alitoa mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya AS Vita Club, sasa anaungana na Al Mahdia inayoshiriki Ligi Kuu ya Libya kuendelea na maisha yake ya soka na kuchangia mafanikio ya klabu hiyo.
Hatua hii inafuatia kuwapoteza wachezaji tegemeo wa klabu ya AS Vita akiwemo Ellie Mpanzu aliyejiunga na Simba SC ya Tanzania na Ikangalombo aliyetimkia Young Africans ya Tanzania. Kumpoteza winga mwingine, Heritier Imana Lote, kunaleta changamoto kwa klabu, lakini pia ni fursa ya kupata wachezaji wengine wenye uwezo wa kuziba nafasi hizo.
Uhamisho huu unaonyesha mabadiliko makubwa ya usajili na wachezaji wanaohama kutoka ligi kuu za Afrika Mashariki hadi Afrika Kaskazini
Pendekezo La Mhariri: