Kai Havertz Kukosa Msimu Ulio Salia Baada ya Kuumia Paja
Kai Havertz Kukosa Msimu Ulio Salia Baada ya Kuumia Paja
Kai Havertz Kukosa Msimu Ulio Salia Baada ya Kuumia Paja | Arsenal imepata pigo kubwa baada ya mshambuliaji Kai Havertz kuumia msuli wa paja alipokuwa mazoezini Dubai. Jeraha hilo lina maana kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atakosa sehemu iliyosalia ya msimu wa 2024-25, na kuacha pengo kubwa katika safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
Vyanzo vya karibu na Havertz vimesema mchezaji huyo anaweza kufanyiwa upasuaji, ingawa Arsenal bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali yake. Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anatarajiwa kupokea ripoti kamili kuhusu ukubwa wa jeraha hilo siku ya Ijumaa kabla ya mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Leicester City Jumamosi.

Kai Havertz Kukosa Msimu Ulio Salia Baada ya Kuumia Paja
Kukosekana kwa Havertz kunaongeza changamoto kwa Arsenal, ambao tayari hawana Gabriel Jesus, ambaye alifanyiwa upasuaji wa goti, na Bukayo Saka, ambaye alifanyiwa upasuaji wa paja baada ya kuumia msuli mwezi Desemba.
Hali hii ina maana kwamba Arsenal italazimika kutegemea wachezaji wengine kwenye kikosi chao au kutafuta suluhu mbadala katika safu ya ushambuliaji ili kusalia katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Pendekezo La Mhariri: