Kapombe Aibuka Nyota wa Mchezo wa Simba vs TZ Prisons 3-0
Kapombe Aibuka Nyota wa Mchezo wa Simba vs TZ Prisons 3-0 | Beki wa kulia wa Simba SC Shomari Kapombe amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi baada ya kutoa pasi mbili za mabao zilizochangia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya TZ Prisons katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara. Ushindi huu umeirudisha Simba SC kileleni mwa msimamo wa ligi.
Kapombe Aibuka Nyota wa Mchezo wa Simba vs TZ Prisons 3-0
Kichapo cha mabao matatu kwa moja kwa Prisons
Simba SC ilionyesha kiwango bora na kufunga mabao matatu kupitia kwa wachezaji wake nyota:
✅ Jean Charles Ahoua alifunga bao la kwanza dakika ya 29 na kumfanya afikishe mabao 8 msimu huu.
✅ Elie Mpanzu Kibisawala aliongeza bao la pili dakika ya 44 na kuandika jina lake kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi hiyo.
✅ Ladaki Chasambi alimaliza dakika ya 45+2, akirekebisha makosa ya mechi iliyopita kwa kufunga bao muhimu.

Kapombe Aibuka Nyota wa Mchezo wa Simba vs TZ Prisons 3-0
Kapombe: Mchango mkubwa kwa Simba SC
Shomari Kapombe alionyesha ubora wake kwa kutoa pasi mbili za mabao, akiendelea kuwa nguzo muhimu kwenye kikosi cha Simba SC. Uwezo wake wa kusaidia katika mashambulizi na kutengeneza nafasi za kufunga umekuwa silaha muhimu kwa Wekundu hao katika kampeni yao ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
Simba SC imerejea kileleni
Kwa ushindi huo Simba SC imefikia hatua muhimu na imerejea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, ikiendelea kuonyesha dhamira ya kutwaa ubingwa.
📌 Matokeo kamili:
🥥 Simba SC 3-0 Prisiones TZ
⚽ 29′ Ahoua
⚽ 44′ Mpanzu
⚽ 45+2′ Chasambi
Pendekezo La Mhariri: