Kilimanjaro Stars Yaaga Kombe la Mapinduzi Baada ya Kipigo
Kilimanjaro Stars Yaaga Kombe la Mapinduzi Baada ya Kipigo cha 2-0 Dhidi ya Kenya
Timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, imeaga mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kupokea kipigo cha pili mfululizo, kikubwa zaidi dhidi ya Kenya, kwa matokeo ya 2-0.
Kilimanjaro Stars Yaaga Kombe la Mapinduzi Baada ya Kipigo
Kipigo hicho cha 2-0 kilikuwa ni cha pili kwa Kilimanjaro Stars, baada ya kukumbana na kipigo cha 1-0 kutoka kwa Zanzibar Heroes katika mechi ya ufunguzi.
Katika mchezo dhidi ya Kenya, Boniface Muchiri alifungua scoring katika dakika ya 56, kabla ya Ryan Ogam kuongeza bao la pili dakika 68, na kuwatumbukiza Kilimanjaro Stars kwenye hali ngumu ya kutimkia nyumbani mapema, bila ya kufuzu kwa hatua inayofuata ya mashindano.
Matokeo ya Mchezo:
- Tanzania (Kilimanjaro Stars) 0-2 Kenya
⚽ 56’ Boniface Muchiri
⚽ 68’ Ryan Ogam
Hata hivyo, licha ya kupoteza michezo miwili, Kilimanjaro Stars bado inatakiwa kucheza mchezo mmoja wa kumalizia ratiba ya Kombe la Mapinduzi, ambapo watakutana na Burkina Faso katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi. Mchezo huu utaamua tu nafasi ya Kilimanjaro Stars katika kundi lao, lakini hauwezi kubadili hatma yao ya kuendelea kwenye mashindano.
Pendekezo la Mhariri: