Kocha wa Geita Gold Augustino Malindi Afungiwa Mechi 16
Kocha wa Geita Gold Augustino Malindi Afungiwa Mechi 16 | Kocha wa makipa wa timu ya Geita Gold, Augustino Malindi, amekumbwa na adhabu kali kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na matukio ya utovu wa nidhamu yaliyotokea wakati wa mchezo kati ya Mbeya City na Geita Gold.
Kocha wa Geita Gold Augustino Malindi Afungiwa Mechi 16
Malindi amefungiwa jumla ya mechi 16 pamoja na faini ya Shilingi Milioni 1 baada ya kumshika sehemu za siri mwamuzi wa akiba wakati wa mchezo huo, tukio lililovunja maadili ya michezo. Kabla ya tukio hilo, kocha huyo alikuwa tayari ameonyeshwa kadi nyekundu kwa kosa la kumtukana mwamuzi msaidizi namba moja (Ass Ref 1).
Hata hivyo, adhabu dhidi ya kocha huyo haikuishia hapo. Akiwa njiani kuelekea vyumbani baada ya kadi nyekundu, alitenda kosa jingine kwa kumshika kifuani mratibu wa mchezo ambaye ni mwanamke, kitendo ambacho pia kimeelezwa kuwa kinyume na maadili ya ukocha na mpira wa miguu kwa ujumla.
Kwa kosa la kumtukana mwamuzi msaidizi wa mchezo huo, Malindi ameongezewa adhabu ya kufungiwa mechi 3 na kupigwa faini ya Shilingi 500,000.
Pendekezo la Mhariri: