Kocha wa KMC Kali Ongala Asema Timu Yake Iko Tayari Dhidi ya Yanga
Kocha wa KMC Kali Ongala Asema Timu Yake Iko Tayari Dhidi ya Yanga | Kocha Mkuu wa KMC FC Kali Ongala amesema kikosi chake kimejipanga vyema kwa ajili ya mechi kali dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC itakayochezwa kesho Februari 14, 2025 kwenye Uwanja wa KMC kuanzia saa 10:00 jioni.
Kocha wa KMC Kali Ongala Asema Timu Yake Iko Tayari Dhidi ya Yanga
Ongala alikiri ubora wa Yanga SC huku akitaja kuwa ni timu yenye bajeti kubwa, wachezaji wa hali ya juu na mashabiki wengi, lakini anaamini KMC inaweza kupata matokeo chanya kwenye mechi hiyo.

Kocha wa KMC Kali Ongala Asema Timu Yake Iko Tayari Dhidi ya Yanga
“Tumejipanga vyema kuwakabili Yanga huko kesho, tunaelewa Yanga ni timu nzuri, wachezaji wanalipwa fedha nyingi, makocha wanalipwa fedha nyingi, wana mashabiki wengi, sisi wengine tunashiriki ligi tu lakini kila timu ina nafasi yake, lolote linaweza kutokea kwa sababu tunaiamini timu yetu na tutapata matokeo,” Ongala alisema.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wa kusisimua, huku KMC ikitaka kupata pointi kubwa dhidi ya Yanga, inayowania kutetea ubingwa wake wa ligi kuu Tanzania bara.
Pendekezo La Mhariri: