Ligi Kuu Kurejea February na Sio Machi Tena
Ligi Kuu Kurejea February na Sio Machi Tena | Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kurejea kwa Ligi kuu ya soka Tanzania Bara katika wiki ya kwanza ya mwezi Februari 2025 kwa michezo ya ‘viporo’ kabla ya kuendelea na michezo ya mzunguko wa 17 ambapo tarehe rasmi pamoja na ratiba iliyofanyiwa maboresho zitatangazwa hivi karibuni.
Ligi Kuu Kurejea February na Sio Machi Tena
Mabadiliko hayo yamekuja baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kusogeza mbele fainali za CHAN kutoka Februari 1, 2025 hadi Agosti, 2025 hivyo kutoa nafasi kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuendelea na michezo ya Ligi Kuu ya NBC ambayo ilisimama kupisha fainali hizo na ilikuwa irejee Machi 2025.
Aidha Bodi ya Ligi imetoa wito kwa klabu zote kuhakikisha zinaongeza nguvu katika maandalizi ya timu zao kiufundi pamoja na masuala mengine hasa yahusuyo miundombinu ya viwanja, ambavyo vitakaguliwa kabla ya kurejea kwa Ligi.
Viwanja vitakavyoonekana kukosa sifa vitaondolewa katika orodha na klabu mwenyeji italazimika kuteua uwanja mwingine miongoni mwa vilivyothibitishwa, kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani.
Pendekezo La Mhariri: