Mahakama Yatoa Wito kwa Wachezaji wa Singida BS Kuhusu Kesi ya Uraia

Filed in Michezo Bongo by on February 14, 2025 0 Comments

Mahakama Yatoa Wito kwa Wachezaji wa Singida BS Kuhusu Kesi ya Uraia | Mahakama kuu kanda ya Dodoma chini ya uongozi wa Jaji Evaristo Longopa imesikiliza kesi inayohusu uraia wa wachezaji wa klabu ya Singida Black Stars leo tarehe 14 Februari 2025.

Mahakama Yatoa Wito kwa Wachezaji wa Singida BS Kuhusu Kesi ya Uraia

Hata hivyo wachezaji hao walishindwa kufika mahakamani kama ilivyotarajiwa na hivyo kusababisha mahakama hiyo kutoa hati ya wito wa kuwaita.

Kwa mujibu wa maagizo ya mahakama, wachezaji wa Singida Black Stars wanapaswa kujibu mashtaka yanayowakabili ifikapo Machi 4, 2025. Hii ina maana kwamba ni lazima wafike na kuwasilisha utetezi wao mahakamani ifikapo tarehe hiyo.

Mahakama Yatoa Wito kwa Wachezaji wa Singida BS Kuhusu Kesi ya Uraia

Mahakama Yatoa Wito kwa Wachezaji wa Singida BS Kuhusu Kesi ya Uraia

Kesi hii imevuta hisia za wadau wa michezo na mashabiki wa soka nchini hasa kutokana na umuhimu wa kipimo cha uraia kwa wachezaji wanaoshiriki Ligi Kuu na mashindano mbalimbali. Wachezaji hao wasipojibu mashitaka hayo kwa wakati hatua zaidi za kisheria zinaweza kuchukuliwa dhidi yao ikiwemo kufungiwa kushiriki ligi kuu Tanzania bara.

Kwa sasa, macho yote yanaelekezwa kwa wachezaji wa Singida Black Stars kuona iwapo watafikishwa mahakamani na kujibu mashtaka kabla ya tarehe iliyopangwa. Uamuzi wa mahakama hiyo hautaathiri tu wachezaji mmoja mmoja, bali pia mustakabali wa klabu yao katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *