Makundi ya AFCON U-17 2025 Tanzania Kundi Moja na Morocco
Makundi ya AFCON U-17 2025 Tanzania Kundi Moja na Morocco | SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetangaza makundi rasmi ya Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON U-17) 2025 zitakazofanyika nchini Morocco.
Droo hiyo imezua shangwe kubwa miongoni mwa mashabiki wa soka barani Afrika huku kila timu ikianza kujiandaa na mchuano huo muhimu wa vijana.
Makundi ya AFCON U-17 2025 Tanzania Kundi Moja na Morocco
Mashindano haya yatahusisha timu 16, ambazo zimegawanywa katika makundi manne kama ifuatavyMakundi ya AFCON U-17 2025 Tanzania Kundi Moja na Morocco/v:
Group A
- ๐ฒ๐ฆ Morocco (Mwenyeji)
- ๐บ๐ฌ Uganda
- ๐น๐ฟ Tanzania
- ๐ฟ๐ฒ Zambia
Tanzania imepangwa kwenye kundi A pamoja na mwenyeji Morocco, timu yenye historia nzuri katika mashindano haya. Uganda na Zambia pia ni wapinzani wenye nguvu ambao wanatarajiwa kuleta ushindani mkubwa.
Group B
- ๐ง๐ซ Burkina Faso
- ๐ดโโ UNIFFAC 1
- ๐ฟ๐ฆ South Africa
- ๐ช๐ฌ Egypt
Egypt na South Africa zinachukuliwa kuwa timu zenye uzoefu mkubwa, huku Burkina Faso nayo ikijulikana kwa vipaji vya vijana wenye uwezo mkubwa wa kushindana.
Group C
- ๐ธ๐ณ Senegal
- ๐ฌ๐ฒ The Gambia
- ๐ธ๐ด Somalia
- ๐น๐ณ Tunisia
Senegal na The Gambia zinafahamika kwa kuzalisha vipaji bora barani Afrika, lakini Somalia na Tunisia pia wanatazamiwa kutoa upinzani mkali.

Makundi ya AFCON U-17 2025 Tanzania Kundi Moja na Morocco
Group D
- ๐ฒ๐ฑ Mali
- ๐ฆ๐ด Angola
- ๐จ๐ฎ Cรดte d’Ivoire
- ๐ดโโ UNIFFAC 2
Mali na Cรดte d’Ivoire ni miongoni mwa timu zenye historia kubwa katika soka la vijana, huku Angola nayo ikiwa na vipaji vikubwa vinavyoweza kushtua wapinzani wao.
Tanzania kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika za U-17 2025
Tanzania imerejea kwenye michuano hiyo baada ya juhudi kubwa kutoka kwa wachezaji wake chipukizi. Kuwa kundi moja na timu za Morocco, Uganda na Zambia ni changamoto, lakini pia ni fursa kwa Serengeti Boys kuonesha umahiri wao kwenye michuano ya kimataifa.
Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Morocco 2025, inatarajiwa kuwa michuano ya kusisimua, timu zote zikilenga kufanya vyema na kufuzu kwa hatua ya mtoano. Tanzania ikiwa ni miongoni mwa washiriki, imepata fursa ya kuweka historia na kufanya vyema dhidi ya wapinzani wao/Makundi ya AFCON U-17 2025 Tanzania Kundi Moja na Morocco.
Pendekezo La Mhariri: