Marcelo Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

Filed in Michezo Bongo by on February 6, 2025 0 Comments

Marcelo Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36 | Nyota wa zamani wa Real Madrid, Marcelo Vieira da Silva Júnior, maarufu kama Marcelo, ametangaza rasmi kustaafu soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 36.

Marcelo Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

Kupitia ujumbe wake kwenye mitandao ya kijamii, Marcelo aliandika:
“Safari yangu kama mchezaji inaishia hapa lakini bado nina mengi ya kufanya kwenye mpira wa miguu. Asante kwa kila kitu.”

Beki huyo wa kushoto alihitimisha safari yake ya soka baada ya kurejea katika timu yake ya utotoni, Flamengo ya Brazil, mnamo Novemba 2024. Marcelo alikuwa na safari ndefu barani Ulaya, akitamba zaidi na Real Madrid ya Uhispania kabla ya kuhamia Olympiacos ya Uturuki mnamo 2023.

Mafanikio ya Marcelo

Marcelo alitajwa kuwa mmoja wa mabenki wa kushoto bora zaidi duniani, akishinda mataji lukuki akiwa na Real Madrid, ikiwemo:

Marcelo Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

Marcelo Atangaza Kustaafu Soka Akiwa na Umri wa Miaka 36

🏆 Mataji 5 ya UEFA Champions League
🏆 Mataji 6 ya La Liga (Ligi Kuu Uhispania)
🏆 Mataji 4 ya Kombe la Dunia la Vilabu

Pia, akiwa na Timu ya Taifa ya Brazil, alicheza mechi 58 na kufunga magoli 6, akiweka rekodi ya kuwa mmoja wa mabeki wa kushoto waliocheza kwa mafanikio makubwa kwa Seleção.

Kustaafu kwa Marcelo kunahitimisha enzi ya mchezaji ambaye alijulikana kwa ujuzi wake wa kudhibiti mpira, kasi, na mchango wake mkubwa katika mafanikio ya Real Madrid. Mashabiki wa soka duniani kote watamkumbuka kama moja ya wachezaji bora wa kizazi chake.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *