Mbosso Afunguka Kuhusu Tetesi za Aslay Kurudi WCB Wasafi

Filed in Burudani by on February 20, 2025 0 Comments

Mbosso Afunguka Kuhusu Tetesi za Aslay Kurudi WCB Wasafi | Mbosso afunguka kuhusu tetesi za Aslay kurudi WCB Wasafi na kutoa maoni yake.

Msanii wa Bongo Fleva Mbosso ameweka wazi maoni yake kuhusu uvumi unaoenea mtandaoni kuwa aliyekuwa msanii mwenzake Aslay anakaribia kujiunga na lebo ya WCB Wasafi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mbosso alisema anawatakia mafanikio wasanii wote, kwa sababu mafanikio ndiyo yanamtoa mtu katika hali ngumu ya maisha.

Mbosso Afunguka Kuhusu Tetesi za Aslay Kurudi WCB Wasafi

“Ukipata nafasi ya kujiunga na WCB Wasafi maana yake ni baraka kubwa. Kwahiyo nawapenda wasanii wote wanaoelekea kwenye mafanikio, mafanikio ndiyo yanatutenganisha na vita dhidi ya umasikini. Kwa hiyo namtakia kila mtu mafanikio, na ikiwa Aslay ana ofa nzuri aende,” Mbosso alisema.

Mbosso Afunguka Kuhusu Tetesi za Aslay Kurudi WCB Wasafi

Mbosso Afunguka Kuhusu Tetesi za Aslay Kurudi WCB Wasafi

Tetesi za Aslay kurejea WCB Wasafi zimekuwa gumzo kwa mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva. Mpaka sasa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa Aslay wala WCB Wasafi kuhusu uwezekano wa kusajiliwa. Mashabiki wa muziki wanabaki na shauku ya kutaka kujua iwapo Aslay atajiunga tena na lebo hiyo maarufu, ambayo iliwahi kuwa chachu ya mafanikio yake alipokuwa sehemu ya Yamoto Band kabla ya kuanza safari ya kujitegemea kimuziki.

Endelea kufuatilia habari zaidi kuhusu mustakabali wa Aslay na uwezekano wa kurudi WCB Wasafi.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *