Mpole Ashinda Kesi Dhidi ya FC Lupopo, Kulipwa Dola 40000

Filed in Michezo Bongo by on January 15, 2025 0 Comments

Mpole Ashinda Kesi Dhidi ya FC Lupopo, Kulipwa Dola 40000

Mpole Ashinda Kesi Dhidi ya FC Lupopo, Kulipwa Dola 40000 | Mshambuliaji wa Pamba Jiji FC George Mpole ameshinda kesi dhidi ya timu yake ya zamani ya FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mahakama imeamuru FC Lupopo kumlipa Mpole fidia ya dola 40,000 sawa na zaidi ya milioni 100 za Kitanzania baada ya kukiuka haki zake za kimkataba.

Mpole aliyejiunga na Pamba Jiji FC baada ya kuachana na FC Lupopo, alikubali kushinda kesi inayohusiana na mkataba wake na mshahara aliodai kuwa hajalipwa ipasavyo na timu hiyo ya DRC. Mahakama ilithibitisha kuwa FC Lupopo ilishindwa kutekeleza baadhi ya masharti ya mkataba wa Mpole, hivyo kulazimika kulipa fidia kubwa.

Mpole Ashinda Kesi Dhidi ya FC Lupopo, Kulipwa Dola 40000

Kwa upande wake George Mpole amekaribisha ushindi huo na kusema kuwa ni hatua muhimu ya kutetea haki za wachezaji na kuhakikisha masharti ya mkataba yanazingatiwa. Mpole alieleza zaidi furaha yake kuona haki inatendeka na sasa anataka kujikita katika mazoezi na maandalizi ya michuano ijayo akiwa na Pamba Jiji FC.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *