Mzize na Aziz Ki Kuhamia Al Ittihad, Yanga Yafikia Makubaliano

Filed in Michezo Bongo by on January 31, 2025 0 Comments

Mzize na Aziz Ki Kuhamia Al Ittihad, Yanga Yafikia Makubaliano | Klabu ya Al Ittihad ya Libya imefikia makubaliano na mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Yanga SC kuwasajili nyota wawili wa timu hiyo Clement Mzize na Stéphane Aziz Ki.

Mzize na Aziz Ki Kuhamia Al Ittihad, Yanga Yafikia Makubaliano

Ofa iliyotolewa na Al Ittihad iliripotiwa kuwa ya kuvutia kiasi kwamba ilikuwa vigumu kwa Yanga kukataa. Hata hivyo pamoja na makubaliano yaliyofikiwa baina ya klabu hizo mbili uhamisho wa wachezaji hao utafanyika rasmi mwezi Juni kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Yanga SC.

Hatua inayofuata kwa Al Ittihad ni kufanya mazungumzo ya kina na wachezaji hao wawili kuhusu mishahara, bonasi na mazingira ya kazi kabla ya kukamilisha uhamisho huo.

Mzize na Aziz Ki Kuhamia Al Ittihad, Yanga Yafikia Makubaliano

Mzize na Aziz Ki Kuhamia Al Ittihad, Yanga Yafikia Makubaliano

Taarifa nyingine zinaonyesha kuwa kati ya wachezaji hao wawili mmoja ameonyesha nia ya kutaka kujiunga na mabingwa hao wa Libya, huku mwingine akiwa na shaka na uhamisho huo. Hali hii inaifanya Al Ittihad kuchukua mazungumzo kwa umakini zaidi ili kuwashawishi nyota hao kujiunga nao msimu ujao.

Mashabiki wa Yanga SC sasa wanasubiri kuona hatima ya wachezaji hawa wawili muhimu, huku wengi wakijiuliza iwapo klabu yao itatafuta warithi wanaofaa endapo wataondoka rasmi.

Pendekezo La Mhariri:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *