Nasreddine Nabi Apewa Kipaumbele Kuwa Kocha Mpya wa Tunisia
Nasreddine Nabi Apewa Kipaumbele Kuwa Kocha Mpya wa Tunisia | Shirikisho la Soka la Tunisia (FTF) limeorodhesha makocha wanne kwa nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa, lakini jina la Nasreddine Nabi limepewa kipaumbele kama chaguo kuu.
Nasreddine Nabi Apewa Kipaumbele Kuwa Kocha Mpya wa Tunisia
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, FTF inatarajia kufanya mawasiliano rasmi na Nabi na klabu yake ya sasa wiki ijayo ili kujadili uwezekano wa kumpa jukumu la kuiongoza Tunisia katika kampeni zao za kimataifa.
Nasreddine Nabi, ambaye amekuwa akihusishwa na mafanikio katika vilabu kadhaa barani Afrika, anaonekana kuwa chaguo sahihi kwa Tunisia kutokana na uzoefu na uelewa wake wa soka la Afrika Kaskazini.
Iwapo mazungumzo hayo yatakamilika kwa mafanikio, Nabi atakuwa na jukumu kubwa la kuiongoza Tunisia katika michuano mikubwa, ikiwa ni pamoja na kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 na mashindano mengine ya CAF.
Mashabiki wa soka nchini Tunisia sasa wanasubiri kwa hamu kuona iwapo Nabi atapambana na kuiongoza timu yake kupata mafanikio.
Pendekezo La Mhariri: