Nejc Gradisar Ajinga na Al Ahly Mkataba wa Miaka Minne na Nusu
Nejc Gradisar Ajinga na Al Ahly Mkataba wa Miaka Minne na Nusu | Nyota wa Fehérvár FC, Nejc Gradisar amekamilisha uhamisho wake kwenda Al Ahly kwa kandarasi ya miaka minne na nusu.
Nejc Gradisar Ajinga na Al Ahly Mkataba wa Miaka Minne na Nusu
Al Ahly italipa Fehérvár FC dola milioni 1.1 kwa huduma ya Gradisar, huku mchezaji huyo akitarajiwa kupokea jumla ya $350,000 katika kipindi cha miezi sita ijayo kama sehemu ya mkataba wake.
Gradisar mwenye umri wa miaka 26, ambaye ameonyesha kiwango kizuri msimu huu, atapokea kandarasi ya jumla ya $700,000 na pia atapokea nyongeza ya $100,000 kutoka 2026. Mkataba huo unamruhusu Gradisar kuwa sehemu ya timu ya mabingwa wa Misri na anatarajiwa fika Cairo kwa uchunguzi wa afya na ujiunge na timu.
Msimu huu, Gradisar amecheza mechi 22, akifunga mabao 8 na kutoa asisti 4, na kuonyesha uwezo mkubwa katika safu ya ushambuliaji.
Al Ahly wanatarajiwa kumtumia Gradisar kuongeza ubora kwenye safu yao ya ushambuliaji, ikiwa ni mkakati wao wa kuendelea kutawala soka la Afrika na kushindana kwa mafanikio makubwa katika mashindano ya kimataifa.
Pendekezo La Mhariri: